Athens. Ugiriki yatangaza hali ya hatari kutokana na maafa ya moto. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Athens. Ugiriki yatangaza hali ya hatari kutokana na maafa ya moto.

Ugiriki imetangaza hali ya hatari nchi nzima baada ya kutokea ajali mbaya kabisa kabisa ya moto msituni ambayo haijawahi kutokea kwa muda wa miongo kadha ambapo kiasi watu 47 wamefariki na kuwazingira wengine wengi katika vijiji.

Wakati maeneo kadha ya rasi ya Peloponnese, kisiwa cha Evia na sehemu ya vitongoji vya mashariki ya jiji la Athens vikiwa vinaungua moto, maelfu ya watu wamekimbia na nyumba kadha pamoja na maeneo ya biashara yameungua moto, pamoja na mamia kadha ya ekari za misitu.

Waziri mkuu Costas Karamanlis amesema jana Jumamosi kuwa moto huo ulioanzia msituni si jambo la ajali tu. Ameahidi kuwa wahusika walioanzisha moto huo watakamatwa na kuadhibiwa, akimaanisha kuwa moto huo umewashwa kwa maksudi na watu waliokuwa na nia ya uharibifu , moto ulioanza kuwaka tangu Ijumaa.

Majimbo yote katika nchi hiyo yametangazwa kuwa ni maeneo ya hali ya hatari ili kuweza kutumia kila kilichopo pamoja na majeshi kukabiliana na maafa hayo. Wanasiasa wamesitisha kampeni zao kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Septemba , bendera zimeamriwa kupandishwa nusu mlingoti kwa ajili ya maombolezo ya muda wa siku tatu na waziri mkuu Karmanlis amesema kuwa Ugiriki inakabiliwa na maafa makubwa ya kitaifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com