Ankara: Mapigano yazuka kati ya majeshi ya Uturuki na waasi wa Kikurdi katika mpaka na Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara: Mapigano yazuka kati ya majeshi ya Uturuki na waasi wa Kikurdi katika mpaka na Iraq.

Kumeripotiwa mapigano kati ya majeshi ya Uturuki na waasi wa Kikurdi karibu na mpaka na Irak. Jeshi la Uturuki limetoa taarifa likisema wanajeshi wake 12 na waasi wa Kikurdi 23 wameuawa katika mapigano hayo. Mapigano yanasemekana yalizuka baada ya waasi wa Kikurdi wa chama cha PKK kuingia Uturuki kutokea kaskazini mwa Irak na kuwashambulia wanajeshi. Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameitisha kikao cha baraza la mawaziri na maafisa wa kijeshi kuzungumzia jinsi ya kujibu shambulio hilo. Shambulio hilo limekuja siku tatu kabla ya bunge la Uturuki kuidhinisha muswada unaoliruhusu jeshi kuwasaka waasi wa PKK katika vituo vyao ndani ya eneo la kaskazini mwa Irak. PKK kimedai kuwakamata mateka wanajeshi kadhaa wa Uturuki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com