Zuma aapishwa.
10 Mei 2009PRETORIA.
Wiki mbili baada ya chama chake cha ANC kushinda katika uchaguzi mkuu, Jacob Zuma ameapishwa kuwa rais mpya wa Afrika Kusini.
Zuma alikula kiapo mbele ya maalfu ya watu, wananchi wa Afrika Kusini na waalikwa kutoka nje.
Rais huyo wa nne tokea kuondolewa mfumo wa kibaguzi nchini Afrika Kusini ametamka kuwa ana wajibu wa kuendeleza malengo ya rais wa awamu ya kwanza ,Nelson Mandela.
Zuma mwenye umri wa miaka 67 amesema daima atatekeleza sera zote zitakazoliendeleza taifa na atayapinga yote yanayoweza kuleta madhara.
Rais huyo mpya pia ameahidi kulinda haki za wananchi wote wa Afrika Kusini na amesisitiza ulazima wa umoja wa watu wote, weusi na weupe katika kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayopaswa kushughulikiwa haraka.
ZA.