1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Papa Benedict Ujerumani

23 Septemba 2011

Baba benedict wa 16 ametoa hotuba ya kihistoria katika bunge nchini Ujerumani, akiwa anaanza ziara ya siku nne katika nchi aliko zaliwa.

https://p.dw.com/p/12exc
Papa Benedict XVI, akiwa amewasili UjerumaniPicha: dapd

Katika hotuba ya dakika 20, Papa aliwaomba wabunge wakumbuke misingi ya ukristo ya uelewa wa sheria barani Ulaya.

Papstbesuch in Deutschland 2011 Berlin
Papa na Kansela Angela Merkel na rais Christian WulffPicha: dapd

Alisema wanasiasa hawapaswi kusahau maadili kwa sababu za uongozi.

Ilkuwa ni hotuba ya kwanza kuwahi kutolewa na papa kwa bunge la Ujerumani. Baada ya kuwasili mjini Berlin hapo jana, alifanya mkutano wa siri na kansela Angela Merkel ambapo walijadili mzozo wa fedha na utandawazi.

Papstbesuch in Deutschland 2011 Berlin
Picha: dapd

Baadaye watu 70,000 walihudhuria misa na kiongozi huyo wa dini katika uwanja wa olimpiki mjini Berlin. Ziara yake inafanyika wakati idadi kubwa ya waumini wa madhehebu ya kikatoliki wamelihama kanisa hilo mwaka uliopita, sehemu ya sababu ikiwa ni mfululizo wa kashfa za ubakaji miongoni mwa viongozi wa kidini.

Mwandishi Maryam Abdalla/dpa, afp, rtr