1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yemen: Waasi waonyesha matumaini baada ya mazungumzo

Lilian Mtono
20 Septemba 2023

Ujumbe wa waasi wa Houthi wa Yemen umerejea mjini Sanaa jana Jumanne baada ya mazungumzo ya siku tano huko Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4WaWG
Waasi wa Yemen wametoa masharti kutaka watumishi wa umma wa Houthi kulipwa mishahara na kuachiwa kwa wafungwa wa Wahouthi
Waasi wa Yemen wametoa masharti kutaka watumishi wa umma wa Houthi kulipwa mishahara na kuachiwa kwa wafungwa wa WahouthiPicha: AP Photo/picture alliance

Mapema leo, Riyadh imesifu matokeo chanya kwenye mazungumzo hayo na waasi ingawa haikutoa maelezo ya kina ya majadiliano hayo yanayolenga kuhitimisha vita vinavyoigharimu pakubwa Yemen.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imekaribisha matokeo hayo chanya yanayolenga kuanzishwa mkakati madhubuti wa kuunga mkono upatikanaji wa amani nchini humo.

Waasi hao wametoa masharti ambayo ni pamoja na watumishi wa umma wa Houthi kulipwa mishahara, kuachiwa kwa wafungwa wa Houthi na kuanzishwa kwa njia mpya kutokea uwanja wa ndege wa Sanaa unaodhibitiwa na Houthi.

Mazungumzo haya ni ishara ya karibuni zaidi inayoibvua matumaini mapya tangu Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulipoivamia Yemen kijeshi mwaka 2015.

Soman Pia:

Saudia yasifu "matokeo chanya" ya mazungumzo na waasi wa Houthi wa Yemen

Waasi wa Huthi wanaoungwa mkono la Iran kwenda Saudi Arabia