1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Saudia yasifu mazungumzo na waasi wa Houthi wa Yemen

20 Septemba 2023

Saudi Arabia imesifu kile imekitaja kuwa "matokeo mazuri" ya mazungumzo yake na waasi wa Houthi wa nchini Yemen ambao walituma ujumbe kwenye taifa hilo la Ghuba kwa majadiliano ya kutafuta amani ya Yemen.

https://p.dw.com/p/4WZxE
Yemen
Mzozo wa Yemen uliozuka mwaka 2014 umesababisha hasara kubwa bila dalili ya kupatikana suluhisho.Picha: Mohammed Huwais/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Saudia kupitia taarifa iliyotoa tathmini ya mazungumzo hayo ya siku tano yaliyowajumuisha wawakilishi wa ngazi ya juu wa waasi wa Houthi .

Taarifa hiyo imesema Saudi Arabia inaendelea kusimama pamoja na Yemen na inazihimiza pande zote kutumia meza ya mazungumzo kutafuta jibu la mzozo wa nchi hiyo

Saudi Arabia imekuwa na dhima kwenye mzozo wa Yemen uliozuka mwaka 2014 kutokana na kuiunga kwake mkono serikali inayotambuliwa kimataifa kwa kufanya mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi.