1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGUN:watawa waendelea na upinzani

25 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMo

Habari kutoka Myanmar zinasema magari ya jeshi yameonekana yakiwa na vipaaza sauti vikitumiwa kutangaza maonyo kwa wananchi wajiweke kando na maandamano ya kuupinga utawala wa kijeshi

Magari hayo yamepitia katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Yangun huku maafisa wakitumia vipaaza sauti hiyvo kuwaambia waandamanaji kuwa hatua zitachukuliwa kwa watu watakaokiuka maonyo yanayotolewa.

Lakini watawa wanaoongoza upinzani dhidi ya serikali ya kijeshi wamesonga mbele na harakati zao leo vilevile.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba hisia za watawala wa kijeshi sasa zinaanza kubadilika. Watawala hao wamesema kuwa sasa utawala unaweza kuwachukulia hatua maalfu ya watawa wanaoongoza upinzani.

Wakati huo huo Ikulu ya Marekani imesema kuwa rais G. W. Bush atauwekea vikwazo zaidi utawala wa kijeshi wa nchini Mynamar ambayo hapo awali ilikuwa inaitwa Burma.