YANGON:Waandamanaji wasakwa na jeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

YANGON:Waandamanaji wasakwa na jeshi

Wanajeshi nchini Myanmar wanatangaza kuwa wanawasaka waandamanaji wanaodai demokrasia katika mji mkuu wan chi hiyo.Kulingana na mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa Marekani nchini humo maafisa wa kijeshi waliwalazimisha watu kutoka majumbani mwao wakati wa usiku.Magari ya kijeshi yalishika doria wakati wa alfajiri huku vipaaza sauti vikitangaza kuwa wana picha na watawakamata wanaohusika.

Shari Vilarosa balozi wa Muda wa marekani nchini Myanmar aliyehojiwa kwa simu anasema kuwa hali ni ya wasiwasi mjini humo.Mjumbe maalum wa Umoja wa Matifa Ibrahim Gambari bado hajatoa maelezo yoyote kuhusu ziara yake ya siku nne nchini humo baada ya utawala wa kijeshi kushambulia waandamanaji katika maandamano ya kudai demokrasia yaliyoongozwa na watawa wa Kibudha.Mamia ya watawa na raia walikamatwa na kupelekwa katika kambi ili kuzuiliwa wakati wa maandamano hayo ya wiki jana.

Japan hii leo kwa upande wake inatangaza kusitisha msaada kwa nchi ya Myanmar kufuatia kupigwa risasi hadi kufa kwa mwandishi mmoja raia wake aliyekuwa akitangaza maandamano hayo mjini Yangon.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com