1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani hii leo

4 Aprili 2006

Magazeti ya Ujerumani hii leo yamejishughulisha na mada mbili zinazohusiana na nishati.Mkutano wa kilele katika ofisi ya kansela mjini Berlin na kadhia ya kansela wa zamani Gerhard Schröder

https://p.dw.com/p/CHWT

Mada mbili zinazohusiana na nishati ndizo zilizohanikiza katika kurasa za magazeti ya Ujerumani hii leo:Mkutano wa viongozi kuhusu nishati uliofanyika katika ofisi ya kansela mjini Berlin na dhamiri za kansela wa zamani kulitumikia kampuni la gesi la Ujerumani na Urusi Gasprom.

Tuanze lakini na mkutano wa kilele wa nishati uliogubikwa na mvutano kati ya vyama ndugu vya CDU/CSU na SPD kuhusu suala la hadi lini nishati ya kinuklea iendelee kutumika humu nchini.

Mhariri wa gazeti la OSTSEE-ZEITUNG la mjini Rostock anaonyesha kavunjwa moyo na mkutano huo.Mhariri anaandika:

„Duru hiyo ya wababe wa kutoka kila upande haikuleta matokeo yoyote ya maana. Bei na kuhakikisha nishati ieendelea kupatikana si mambo yanyoweza kushawishiwa kwa uamuzi wa serikali ya shirikisho.Ni suala linaloyahusu makampuni ya kimataifa.

Makampuni manne makubwa ya nisharti humu nchini yanaendelea kufaidika na biashara hiyo inayomilikiwa na walio wachache.Soko huru ni jengine kabisa.Kwa hivyo si hasha washirika katika serikali ya muungano yaani CDU/CSU na SPD wanaposhindwa kulipatia jibu suala tete-„eti unaionaje nishati ya kinuklea?“.

Gazeti la Landeszeitung la mjini Lüneburg linashangiria angalao suala la siasa ya nishati limerrejea katika meza ya majadiliano.

„Mkutano wa kilele kuhusu nishati ungestahiki uitishwe tangu zamani.Ruuya za kisiasa humu nchini zinatuwama zaidi katika masuala ya kodi au kufanya kazi dakika 18 zaidi ya muda uliopangwa.Hoja kwamba enzi za mafuta yanayochimbwa ardhini zimepita,hakuna anaezitilia maanani.Mkutano wa kilele wa nisharti hauwezi kuyapatia jibu matatizo yaliyopo-lakini angalao umewazindua wananchi.

Gazeti la mjini Berlin TAGESSPIEGEL linazungumzia madhara ya kuachana na nishati ya kinuklea.Gazeti linaandika:

„Ingawa matumizi ya nishati yamepungua nchini Ujerumani lakini bado watu wanategemea nishati kutoka nje.Zamani tulikua tukitoa petro dolla kuwagharimia waimla wakiarabu waliokua wakieneza itikadi kali za dini ya kiislam.

Hii leo fedha hizo zinamiminika Rashia ambako Vladimir Putin anaendelea kukandamiza haki za binaadam,kuvunja uhuru wa vyombo vya habari na kuwafumba midomo wapinzani.Tunaupatia nguvu utawala unaoangamiza maisha ya watu katika Tchechnya,unaoiwekea vikwazo vya gesi Ukraine na kulishawishi eneo la mashariki la kati lizigeukie nchi za magharibi.Serikali ya zamani ya muungano wa nyekundu na kijani imetutafutia mashaka ilipoamua kuachana na matumizi ya nishati ya kinuklea na kuikumbatia Moscow badala yake.

Hoja za Berliner TAGESSPIEGEL zinatufikisha katika mada yetu ya pili magazetini.

Korti ya mjini Hambourg imemkataza kiongozi wa chama cha FDP Guido Westerwelle asimsingizie Gerhard Schröder,eti alipokua kansela wa Ujerumani aliingilia kati ili kampuni la gesi la Urusi Gasprom lipatiwe mkataba wa kujenga mabomba ya kusafirishia gesi ya Urusi hadi Ujerumani kupitia bahari ya Baltik.Licha ya hukmu hiyo ugonvi wa Schröder unaendelea.

Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linaandika:

„Kadhia ya Schröder na uongozi wa kampuni la gesi ina ncha mbili zinazotatanisha:kwanza siasa ya nje inayofungamanishwa na siasa ya kiuchumi na nishati na pili hadhi ya kansela huyo wa zamani.

Kwamba suala hilo la pili ndio chanzo cha watu kwenda mahakamani na kuzusha uwezekano wa kuundwa kamisheni ya uchunguzi ya bunge,si jambo linalobidi kumstaajabisha mtu mwenye kupenda madaraka kama Schröder.

Ameuvalia njuga mradi wa kupatiwa Ujerumani gesi toka Rashia,kupitia bahari ya Baltik bila ya kuwajali washirika wake ndani ya umoja wa ulaya .Na zaidi ya yote hayo anachaguliwa kua mwenyekiti wa baraza la usimamizi.Si hasha kwa hivyo watu wakimtilia shaka.Suala kama kumekua na udhamini wa benki ya Ujerumani au la si muhimu,pekee dhana kwamba mambo ya kibinafsi yamegeuzwa kua ya kiserikali inatia aibu.