WIESBADEN: Mauzo ya nje ya Ujerumani yavunja rekodi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WIESBADEN: Mauzo ya nje ya Ujerumani yavunja rekodi

Ongezeko kubwa la mauzo ya nje katika mwaka 2006 la Euro bilioni 162 limesaidia kuweka rekodi ya biashara ya kigeni ya Ujerumani.Kwa mujibu wa Idara ya Takwimu ya Ujerumani,kampuni za Kijerumani mwaka jana ziliuza nchi za ngámbo bidhaa zenye thamani ya Euro bilioni 893.Kwa mara nyingine tena,washirika wakuu kibiashara ni nchi za Umoja wa Ulaya.Mwaka jana,mauuzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 13.7 na hivyo Ujerumani imeshika nafasi ya kwanza kama msafirishaji mkuu wa bidhaa duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com