1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WEISBADEN : Ujerumani haikupanga siku ya kutoka Bosnia

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCN2

Ujerumani imetupilia mbali tetesi kwamba imepanga tarehe ya kuondowa wanajeshi wake 850 kutoka Bosnia.

Kufuatia mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya mjini Wiesbaden nchini Ujerumani waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba Ujerumani ilikuwa ikiangalia hali ilivyo lakini haikuamuwa hatua za kuchukua baada ya hapo.

Gazeti la Financial Times kwa kumtaja mwandiplomasia mmoja wa Umoja wa Ulaya limeripoti kwamba Ujerumani ilikuwa ikijiandaa kufuata hatua ya Uingereza kuondowa vikosi vyake kutoka Bosnia.

Serikali ya Uingereza ilitangaza hapo Alhamisi kwamba itaondowa zaidi ya wanajeshi wake 600 kutoka jimbo hilo la Balkan kutokana na hali ya usalama kuwa nzuri.