Watu kuwa na njaa katika dunia iliotajirika | Masuala ya Jamii | DW | 30.10.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Watu kuwa na njaa katika dunia iliotajirika

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa haijapungua tokea miaka ya 90 licha ya kwamba dunia imetajirika ukilinganisha na hali ilivyokuwa miaka 10 iliopita. Idadi ya watu wenye kuwa na njaa imeongezeka kwa milioni 4 kila mwaka. Hivyo ni kulingana na ripoti ya kila mwaka ya shirika la chakula na kilimo duiniani FAO.

Mama na mwanae nchini Ethiopia

Mama na mwanae nchini Ethiopia

Katika ripoti ya shirika chakula na kilimo duniani FAO, mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo, Jacques Diouf, amesema katika dunia ya leo kuna watu milioni 854 wanaokabiliwa na njaa ambapo milioni 820 wanapatikana katika nchi maskini ambazo wakati mwingine hutajwa nchi zinazoendelea.

Mnamo mwaka wa 1996 wakati wa mkutano wa kilele juu ya chakula duniani uliofanyika mjini roma Italy, makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO, dunia ilikuwa na lengo muhimu la kupunguza hadi nusu idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa duniani kikizingatiwa kipindi cha miaka 1990-92, ilikuwa ni sawa na watu milioni 412.

Lakini Jacques Diouf amesema, miaka 10 baadae, tumejikuta katika hali kwamba hakuna maendeleo yoyote yaliofikiwa kuelekea lengo hilo.

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kwa hakika ni ndogo lakini ukizingatia tarakwim, amezidi kusema Jacques Diouf, hakuna mabadiliko yaliyotokea. Kwani amesema idadi ya watu wanaokaa na njaa kupungua kwa milioni tatu tu yaani kutoka milioni 823 hadi milioni 820, huenda likawa ni kosa tu katika mahesabu na wala sio mabadiliko ya kusherehekea.

Mbali na watu wenye kuwa na njaa, watu wanaopata chakula ambacho hakitoshi au wale wanaokula vibaya, wameongezeka pia ukizingatia miaka ya 1995-97 hadi miaka ya 2001-2003, hali imezidi kuwa mbaya kwani idadi hiyo ilikuwa imepunguwa kwa watu milioni 100 miaka ya 1980.

La kustajabisha anasema Jacques Diouf, mkurugenzi wa shirika la chakula na kilimo duniani, dunia imetajirika kuliko ilivyokuwa miaka 10 ya nyuma. Chakula kimeongezeka . Kinachokosekana ni nia na utashi wa viongozi wa kutoa fedha kwa ajili ya wale wanaokabiliwa na njaa.

Wataalamu wanasema tarakwim kuhusiana na hali ya njaa duniani ni za kuzingatiwa kwa makini. Shirika la chakula na kilimo duniani FAO, linakisia kuwa hadi kufikia mwaka wa 2015, idadi ya watu wenye kukaa na njaa, itapungua hadi kufikia watu milioni 582, sawa na upungufu wa milioni zaidi ya milioni 200 ukilinganisha na hali ya sasa hivi.

Hiyo haitowi hali halisi ya mambo. Kwa mfano wanasema wataalamu hao, idadi ya watu wanaokaa na njaa ilipungua bara za Ashia na Pacifik, lakini tarakwim zilishushwa na hali katika nchi mbili tu: Uchina na Vietnam ambako wakulima walinufaika na hali ya uzarishaji mkubwa na hivyo raia takriban wote na hata wanavijiji wakapata chakula cha kutosha. Lakini katika nchi zingine zote katika maeneo hayo, ilizidi kuwa mbaya.

Barani Afrika na hususan chini ya jangwa la Sahara, ugonjwa wa ukimwi , vita na majanga kama mafuriko, vilikwamisha juhudi za serikali za kupambana na njaa kama vile nchini Burundi, Eritrea, Liberia, Sierra Leonne na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kulingana na shirika la chakula na kilimo duniani FAO, njia bora ya kukomesha njaa duniani ni kupambana na umaskini.

 • Tarehe 30.10.2006
 • Mwandishi Gregoire Nijimbere
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHmD
 • Tarehe 30.10.2006
 • Mwandishi Gregoire Nijimbere
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHmD

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com