1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 5 wapigwa risasi na kuuwawa na polisi Watamu Kenya

31 Machi 2010

Watu wengine 17 wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi

https://p.dw.com/p/MjS6

Nchini Kenya watu watano wameuawa na wengine wasiopungua 17 kulazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi, kufuatia vurugu iliotokea baina ya wanakijiji wa Watamu mjini Malindi na maafisa wa usalama.

Wingu la simanzi lilitanda katika kijiji hicho maarufu sana kwa shughuli za kitalii wakati wa maziko ya baadhi ya waliouawa.