1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Isaac Gamba
27 Desemba 2016

Mapigano yaliyofanyika kati ya makundi ya wanamgambo katika vijiji vya Kivu Kaskazini, yameua watu 35 wakati wa kipindi cha Krismasi. Ni eneo lenye idadi kubwa ya Wakiristo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/2UuWd
Demokratische Republik Kongo Straßenszene in Kinshasa
Picha: DW/P. Chitera

Mauaji ya watu yalifanyika katika mji wa Eringeti, ulioko kilomita 55 kaskazini mwa mkoa wa Beni ambao kwa kipindi cha miaka miwili umekuwa katika machafuko yaliyowaua mamia ya watu.  Waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF), waliwaua watu 22 baada ya kuvamia mji wa Eringeti Jumamosi iliyopita. Afisa mmoja wa eneo hilo, Amisi Kalonda, alilieleza shirika la habari la AFP.  Idadi ya vifo iliongezeka na kufikia 35 hapo jana  baada ya kupatikana taarifa kuwa kiasi ya watu  13 wa kabila la Hutu wengi wao wakiwa ni wanawake na mtoto wa kike wa umri wa miaka minane waliuawa hapo Jumapili na wapiganaji wa kabila la Nande. Watu wa kabila la Nande na makabila mengine nchini humo, wanawachukulia Wahutu kama wageni kwa sababu ya kujiambatanisha kwao na kabila lenye watu wengi katika nchi ya jirani ya Rwanda.