WASHINGTON:Rais Bush na Saad Hariri kukutana | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Rais Bush na Saad Hariri kukutana

Rais George Bush wa Marekani na kiongozi wa bunge la Lebanon Saad Hariri wanatarajiwa kufanya mazungumzo hii leo kujadilia hali nchini humo pamoja na ushawishi wa nchi jirani ya Syria.Viongozi hao wawili aidha wanatarajiwa kuzungumzia uchaguzi wa rais ujao wa Lebanon huku Marekani ikiahidi kushirikiana na kiongozi atakayeteuliwa kwa njia ya uhuru.

Mauaji ya kisiasa yamekumba Lebanon kikiwemo kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Rafiq Hariri aliyeuawa mwaka 2005 aidha mwanasiasa anayepinga Syria Antoine Ghanem mwezi jana.Bunge la Lebanon liliahirishwa hadi Oktoba 23 kwa ukosefu wa wabunge wa kutosha kushiriki katika shughuli ya uchaguzi wa rais.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com