1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Iran na Marekani kufanya mazungumzo.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2A

Marekani na Iran zinapanga kufanya mazungumzo ya kihistoria katika muda wa wiki chache zijazo kujali hali ya usalama nchini Iraq.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Gordon Johndroe amethibitisha tangazo kuhusu mkutano huo ambao wizara ya mambo ya kigeni ya Iran ilitoa jana Jumapili.

Johndroe amesema nia ya mkutano huo ambao utafanyika mjini Baghdad itakuwa ni kuona jinsi gani Iran inaweza kutoa mchango wake kwa usalama nchini Iraq.

Marekani amekuwa ikiishutumu Iran katika siku za nyuma kwa kuwa jirani mharibifu wa Iraq.

Marekani na Iran hazijakuwa na uhusiano wa kidiplomasia kwa zaidi ya miaka 25.