WASHINGTON:Bush ataka fedha zaidi kwa wanajeshi wake Iraq na Afghanstan | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Bush ataka fedha zaidi kwa wanajeshi wake Iraq na Afghanstan

Rais George W Bush wa Marekani amelitaka Bunge kuidhinisha kiasi cha dolla billioni 200 za kugharamia shughuli za kijeshi mwaka ujao.

Akitoa wito huo kwa bunge hapo jana rais Bush amesema.

*Nakubaliana kwa dhati kwamba lazima tuwape wanajeshi wetu usaidizi wanaouhitaji kutekeleza kazi zao.Marekani lazima ifanye kila iwezalo kuwasaidia wanajeshi wake na kuwalinda wananchi wake na hivyo nalitolea mwito bunge kuidhinisha fedha zitakazofanikisha suala hilo*

Fedha hizo zinategemewa kutumika katika shughuli za vita nchini Iraq na Afghanstan mwaka 2008.

Endapo bunge litaidhinisha fedha hizo basi gharama ya vita itapindukia dollar billioni 750 tangu rais Bush alipoanzisha kile kinachojulikana kama vita dhidi ya Ugaidi tangu kutokea mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com