1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Bush aahidi kushirikiana na chama cha Democrats.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuF

Rais wa Marekani George W. Bush amesema yuko tayari kuzingatia mashauri kutoka katika chama kinachoongoza katika baraza la Congress juu ya kushinda vita nchini Iraq.

Bush amesema hawezi kubadili mawazo kuhusu lengo lake la “ushindi“ nchini Iraq, anaouelezea kwamba hadi pale Iraq itakapoweza kujihami na kujitawala wenyewe.

Aidha Rais Bush ameendelea kukataa mwito ratiba ya kulirejesha nyumbani jeshi la Marakani lililopo nchini Iraq.

Wakati huo huo jeshi la Marekani hii leo limetangaza vifo vya wanajeshi wake wawili na mwanamaji mmoja nchini Iraq, na kupelekea kuongezeka idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa nchini humo mwezi huu kufikia 23.