Washington. Tony na Bush kubadili mwelekeo wa sera zao kuelekea mashariki ya kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Tony na Bush kubadili mwelekeo wa sera zao kuelekea mashariki ya kati.

Rais wa Marekani George W. Bush na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair wamesema kuwa watatathmini upya sera zao kuelekea mashariki ya kati. Hii inakuja baada ya mkutano baina ya viongozi hao wawili mjini Washington baada ya kutolewa tathmini na jopo la wanasiasa waandamizi nchini Marekani kuhusiana na hali nchini Iraq.

Blair na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice wanatarajiwa kwenda mashariki ya kati hivi karibuni katika juhudi za kufufua mazungumzo ya amani kati ya Waisrael na Wapalestina.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kuwa wako tayari kuangalia upya sera zao na kwamba ripoti ya jopo lililoongozwa na waziri wa mambo ya kigeni wa zamani wa Marekani James Barker inatoa mwanga wa wapi pa kuelekea.

O-Ton Blair.

Kwa upande wake rais George W. Bush amesema kuwa taarifa hiyo ya James Barker itaangaliwa kwa makini.

O-Ton Bush

Katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani, Bwana Bush amekiri kuwa hali nchini Iraq ni mbaya, lakini amesema kuwa anasubiri ripoti mbili nyingine kutoka wizara ya ulinzi na wizara ya mambo ya kigeni. Blair na Bush wamesema kuwa mapendekezo ya kundi lililofanya tathmini ya hali nchini Iraq ya kutaka kufanya mazungumzo moja kwa moja na Iran na Syria yatawezekana tu iwapo nchi hizo zinasitisha kuunga kwao mkono watu wenye msimamo mkali na kuiunga mkono serikali ya mjini Baghdad inayolegalega.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com