WASHINGTON: Sheria irekebishwe kuambatana na teknolojia | Habari za Ulimwengu | DW | 29.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Sheria irekebishwe kuambatana na teknolojia

Rais wa Marekani,George W.Bush ametoa wito kwa Bunge kuregeza vikwazo vya kuwachunguza washukiwa ugaidi.Katika hotuba yake ya kila juma kwenye redio,Bush aliwahimiza wabunge waidhinishe sheria ya FISA ya mwaka 1978 inayohusika na utaratibu wa upelelezi ambayo imefanyiwa marekebisho kulingana na hali ya sasa.Bush amesema,magaidi wanatumia teknolojia ya kisasa kama vile simu za mkono na mtandao wa Internet.

Mswada wa sheria uliopendekezwa na Ikulu ya Washington katika mwezi wa Aprili,unataka kuregeza vikwazo ili kuruhusu kudaka barua pepe, mazungumzo ya simu na mawasiliano mengine nchini Marekani.Wabunge wa chama cha Demokratik wamesema,wao hawatoidhinisha marekebisho hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com