1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rice na Steinmeier wajadili suala la Irak

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl2

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice,kwa mara nyingine tena amepinga kuwa na majadiliano ya uso kwa uso na Syria na Iran, kutenzua mgogoro wa Irak.Baada ya kukutana na waziri wa nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier mjini Washington,Rice alisema nchi hizo mbili zinachochea siasa kali.Kwa matamshi hayo,yadhihirika kuwa Rice anapinga pendekezo kuu la Halmashauri ya Baker kuhusu njia mpya za kupata suluhisho la kuleta usalama nchini Irak.