WASHINGTON : Mswada wa azimio la Iran waungwa mkono na Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Mswada wa azimio la Iran waungwa mkono na Marekani

Marekani imetia saini mswada wa azimio uliopendekezwa na nchi za Ulaya kuiwekea Iran vikwazo kuhusika na mradi wake wa nyuklia.Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice amesema,ni matumaini yake kuwa mswada huo utapitishwa kwa haraka katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Azma ya vikwazo hivyo vinavyoweza kuanza kufanya kazi kabla ya mwisho wa mwaka huu,ni kuishinikiza Iran kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com