Washington. Marekani yatoa wito wa kutozidisha hali ya wasi wasi. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Marekani yatoa wito wa kutozidisha hali ya wasi wasi.

Marekani jana imezitaka Eritrea na Ethiopia kutoongeza hali ya wasi wasi katika nchi jirani ya Somalia lakini zijaribu kutafuta njia muafaka kuelekea nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita ya pembe ya Afrika.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Sean McCormack amesema kuwa Marekani inaangalia kwa karibu kile kinachotokea nchini Somalia, ambako serikali ya mpito imeushutumu muungano wa mahakama za Kiislamu kwa kuwakamata wabunge wake watatu jana Alhamis.

Muungano huo wa mahakama za Kiislamu ambao wameukamata mji mkuu wa Mogadishu mwezi wa Juni na wanadhibiti maeneo mengine muhimu, umekana kuwakamata wabunge hao na kusema kuwa walikuwa wanajaribu kuwalinda dhidi ya majeshi ya Ethiopia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com