1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Makubaliano mapya kati ya Marekani na Chad

Makubaliano yaliopatikana kati ya Marekani na Chad yanafungua njia ya kuipatia Chad msaada wa kijeshi ikiwa ni pamoja na silaha za ulinzi kutoka Marekani.Hapo awali,ilikuwa marufuku kuipa Chad msaada wa aina hiyo sawa na zile nchi zinazokataa kuwakinga Wamarekani dhidi ya uwezekano wa kupelekwa mbele ya Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa-ICC.Kuambatana na makubaliano yaliopatikana,Mahakama ya Uhalifu haitokuwa na mamlaka ya kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya Wamarekani katika ardhi ya Chad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com