1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Lawama kali za rushwa kuhusu polisi wa Irak

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSA

Vikosi vya Irak havitoweza kulinda usalama wa nchi katika kipindi kijacho cha miezi 12 hadi 18.Hilo ni hitimisho la ripoti mpya iliyowasilishwa katika bunge la Marekani mjini Washington. Jemadari mstaafu wa vikosi vya wanamaji,James Jones alieongoza tume ya watu 20 amesema,wizara ya mambo ya ndani ya Irak haifanyi kazi na ina umadhehebu.Kwa maoni ya tume hiyo,vikosi vya polisi vya Irak vinapswa kupangwa upya.Maafisa wapotovu na wale wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya kimadhehebu,wanapaswa kufukuzwa.

Idadi ya wanasiasa wa Kimarekani wanaotaka vikosi vyao virejeshwe nyumbani,inazidi kuongezeka.Juma lijalo,kamanda wa majeshi ya Marekani huko Irak, Jemadari David Petraues,anatazamiwa kuwasilisha katika bunge la Marekani,ripoti juu ya maendeleo ya operesheni ya nchini Irak.