WASHINGTON: Gates amekosoa azimio lililopitishwa na Seneti | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Gates amekosoa azimio lililopitishwa na Seneti

Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates amekosoa azimio la Seneti linalopinga mpango wa rais George W.Bush kupeleka vikosi zaidi nchini Irak.Katika mkutano wake wa kwanza pamoja na waandishi wa habari tangu kuchukua nafasi ya Donald Rumsfeld kama waziri wa ulinzi Desemba mwaka jana,Gates alisema,azimio hilo ambalo halina uzito wa kutekelezwa,litawatia moyo maadui nchini Irak.Kwa upande mwingine,rais Bush amesisitiza kuwa yeye ndio anaepitisha maamuzi na kwamba yatakuwa maafa makubwa kwa Marekani ikiwa ushindi hautopatikana nchini Irak.Na kuhusu Iran,Bush hajakanusha ripoti za gazeti la “Washington Post“ kuwa vikosi vya Marekani vina mamlaka ya kuwakamata au kuwaaua mawakala wa Kiirani nchini Irak wanaoaminiwa kuwa ni hatari kwa usalama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com