1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush anakutana na viongozi wa Demokrat

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCto

Rais George W.Bush wa Marekani amekutana na viongozi wengine wa chama cha upinzani cha Democrat,baada ya chame chake cha Republikan kushindwa uchaguzi wa mabaraza yote mawili ya bunge.Bush amekuwa na mazungumzo na Harry Reid anaekiongoza chama cha Demokrat katika Seneti. Reid anatazamiwa kuongoza Seneti,chama cha Demokrats kitakaposhika madaraka ya baraza hilo katika mwezi wa Januari.Siku ya Alkhamisi,Bush alikutana pia na Nancy Pelosi anaetarajiwa kuliongoza Baraza la wawakilishi.