1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Brown akutana na Bush kwa mara ya kwanza.

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdW

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown yuko nchini Marekani kwa mazungumzo yake ya kwanza na rais George W. Bush tangu kuingia madarakani mwezi uliopita.

Kufuatia mazungumzo yao katika eneo la mapumziko la rais la Camp David, waziri mkuu Brown amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini kuwa mahusiano ambayo tayari ni mazuri kati ya Uingereza na Marekani yataimarika zaidi hapo baadaye.

Pia ameainisha kile anachofikiri kuwa ni masuala muhimu ya sera za mambo ya kigeni kwa nchi hizo mbili.

Katika suala la majeshi ya Uingereza nchini Iraq Brown amesema kuwa ,

lengo letu kama lilivyo lile la Marekani ni kusogea hatua kwa hatua katika kutoa udhibiti kwa maafisa wa Iraq, kwa serikali ya Iraq na majeshi yake ya ulinzi wakati hatua za maendeleo zikifikiwa. Na tunaondoka kutoka katika hatua za mapambano hadi katika uangalizi , katika mikoa mitatu kati ya minne ambapo majeshi ya Uingereza yana jukumu la ulinzi wa usalama.

Brown pia anatarajiwa kukutana na viongozi wa vyama vya Republican na Democratic katika baraza la Seneti na baraza la wawakilishi kabla ya kusafiri kwenda mjini New York ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon na kuhutubia halmashauri kuu ya umoja huo.