1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warusi na walimwengu wamuaga Boris Yeltzin

Oummilkheir24 Aprili 2007

Sifa za kila aina kwa kiongozi wa zamani wa Urusi aliyefariki dunia jana

https://p.dw.com/p/CB4U
Boris Yeltzin amepanda kifaru kutangaza kushindwa njama ya mapinduzi
Boris Yeltzin amepanda kifaru kutangaza kushindwa njama ya mapinduziPicha: AP

.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amemsifu mtangulizi wake kwa kusema:

“Mchango wake,kila mmoja anaweza kuutathmini atakavyo.Lakini kimoja ni dhahiri:Ilikua chini ya utawala wa Boris Yeltzin,ambapo wananchi wa Urusi walifanikiwa kujipatia cha muhimu kuliko yote:uhuru.Hiyo ni jaza ya kihistoria kwa Boris Yeltzin.”

Enzi mpya imeibuka ,enzi ya Urusi ya kidemokrasi-ameongeza kusema kiongozi huyo wa Urusi.

Boris Yeltzin atazikwa kesho katika kiunga kimoja cha mjini Moscow alikozikwa pia waziri mkuu wa enzi za kikoministi Nikita Khrouchtchev. Ikulu ya Urusi-Kremlin imetangaza siku moja ya maombolezi kote nchini humo.

Kuanzia leo maiti ya Boris Yeltzin imewekwa katika kanisa kuu la mjini Moscow-lililojengwa baada ya kuporomoka enzi za kikoministi ambako Warusi wameanza kumiminika kumpa heshma za mwisho kiongozi wao wa zamani.

Rais George W. Bush wa Marekani amesifu mchango mkubwa wa rais Boris Yeltzin katika kuuvunja pingu za enzi za kikoministi.Katika taarifa yake rais Bush amesema :,

“Laura na mie binafsi tumesikitishwa sana na kifo cha rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltzin.Ameingia katika madaftari ya historia kwa kuleta mageuzi ya kimsingi na ya maana nchini mwake.Amechangia sana katika kuporomosha enzi za usovieti-amechangia kuleta uhuru na alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia za kidemokrasi .Nnashukuria juhudi za rais Boris Yeltzin za kuanzisha uhusiano madhubuti kati ya Urusi na Marekani.”

Waziri mkuu wa Uengereza Tony Blair amemsifu kiongozi huyo wa zamani wa Urusi pamoja na mchango muhimu alioutoa kwa nchi yake.Waziri mkuu wa zamani wa Uengereza Margreth Thatcher amesema Boris Yeltzin anastahiki kusifiwa kama “mzalendo na mkombozi.”

Kansela Angela Merkel, ambae nchi yake ndio mwenyekiti wa umoja wa ulaya amesema:

“Nimetuma rambi rambi na nnastahiki kusema kwamba Boris Yeltzin ni mpiganiaji thabiti wa uhuru na demokrasia nchini mwake.Alikua rafiki wa dhati wa Ujerumani.Vikosi vya Usovieti ya zamani vimerejea nyumbani kwasababu yake na ndio maana daima wajerumani watamkumbuka kama rafiki wa kweli.”

Kansela wa muungano wa ujerumani Helmut Kohl amemsifu “ mwandani wa kweli wa wajerumani.Hakuna sifa zinazoweza kushadidia mchango wake katika kuinua uhusiano kati ya Ujerumani na Urusi na amani ulimwenguni” amesisitiza kansela huyo wa zamani wa Ujerumani Dr. Helmut Kohl.