1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wanne wauwawa na mashambulizi ya Israel

3 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cjmo

GAZA CITY

Wapalestina wanne wameuwawa katika mashambulizi ya anga na ardhini ya Israel katika Ukanda wa Gaza leo hii.

Wanajeshi wa Israel wakisaidiwa na vifaru na helikopta za kivita wamekuwa wakiendesha operesheni yao hiyo katika kijiji cha Bani Suheila karibu na mji wa kusini wa Khan Yunis.

Wapiganaji watatu wa Kipalestina na mwanamke mmoja wameuwawa na wengine 30 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya Israel ambayo ni ya karibuni kabisa dhidi ya Ukanda wa Gaza unaotawaliwa na kundi la Hamas.