Wapalastina: Hamas na Fatah wazidi kuhasimiana | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 12.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Wapalastina: Hamas na Fatah wazidi kuhasimiana

Rais Mahmoud Abbas wa Palastina (kushoto) na waziri mkuu, Ismail Haniya

Ile amri ya kusitisha mapigano iliokubaliwa juzi baina ya vyama vya Wapalastina vya Hamas na Fatah haijadumu. Badala yake utumiaji nguvu umezuka upya baina ya makundi hayo ya Wapalastina yanayohasimiana. Jana asubuhi nyumba ya waziri mkuu Ismail Haniya ilishambuliwa, na jioni ya siku ya kabla wapiganaji wa chama cha Hamas walimuuwa katibu mkuu wa chama cha Fatah kaskazini mwa Ukanda wa Gaza pamoja ndugu yake. Peke yake siku ya jumatatu mapigano hayo yalichukuwa roho za watu 14, na hofu imetanda miongoni mwa watu katika Ukanda wa Gaza. Katika hali kama hiyo mtu hawezi kuzungumzia juu ya kuunda dola.

Huko Gaza limekuwa ni jambo la kupoteza wakati kuhesabu kama usitishaji wa mapigano utaheshimiwa ama hautaheshimiwa. Ikiwa saa moja imepita bila ya kuvunjika mapatano yaliokubaliwa hapo kabla ya kusitisha mapigano, basi jambo hilo litatathminiwa kuwa ni mafanikio. Kile ambacho Wapalastina katika Ukanda wa Gaza na huenda karibuni pia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wanachofanya, bila ya shaka, ni mtihani mkubwa kwa huruma na nia njema iliooneshwa hadi sasa na watu wengi duniani. Kutokana na risasi zinazofyetuliwa, mapambano, utekaji nyara na vitendo vingine vya utumiaji nguvu vinavofanyika huko Gaza kuna hofu ya kuharibika ile huruma na majonzi waliokuwa nayo watu kuelekea Wapalastina, na ile haki yao kubadilishwa na watu watakaosema: Wapalastina hawawezi kuwa na dola.

Umwagaji wa damu wa siku na wiki chache zilizopita haujahusiana na vitendo vya Wa-Israeli. Hapa suala la mwanzo ni mapambano ya kuwania madaraka, na sio kwamba suala la mbele kabisa ni malumbano juu ya nani aliye na nadharia ilio bora au mkakati ulio bora, lakini suala ni moja na pekee: nalo nani sasa mwenye usemi miongoni mwa Wapalastina. Chama cha Fatah, kinachoongozwa na rais wa Wapalastina, Mahmoud Abbas, bado hakiko tayari kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa mwanzo wa mwaka jana ambao ulikiweka madarakani chama cha Hamas. Hapa si suala sio kama Chama cha Hamas siku moja hakitabidi kiwe tayari kuitambua Israel, lakini hapa suala ni la kupilizana visasi vya zamani na vipya. Haya ni mabishano ambayo yalitanzuiliwa mbele ya meza ya mashauriano huko Kairo, Damascuss na Riyadh, lakini baadae yakafumka tena na utumiaji nguvu ukafuata mabarabarani. Jambo la kipuuzi ni kwamba pande zote hizo mbili, yaani vyama vya Hamas na Fatah, vimo ndani ya serekali moja waliokubaliana kutokana na ushauri wa Saudi Arabia. Kutokana na wawakilishi wa Chama cha Fatah kushiriki katika serekali hiyo, dunia ilidanyganyika kwamba serekali hiyo itakuwa na sura ya kutaka masikilizano.

Hiyo ilikuwa mbinu ambayo karibu ingefaulu. Katika nchi za nje watu walishughulika tu kuutizama msimamo wa Chama cha Hamas kuelekea Israel, lakini baadae watu hao hao walikuwa na furaha kwamba sasa mtu ataweza kuzungumza na watu wenye misimamo ya wastani kama vile Mahmoud Abbas na wanasiasa wengine wa Chama cha Fatah. Mapigano ya sasa katika Gaza na mzozano wa sasa baina ya washirika wa serekali ya mseto wasiokuwa sawa inafanya kusiweko matumaini, hasa wakati huu ambapo Umoja wa Ulaya umeamua kurejesha tena misaada yake rasmi kwa Wapalastina. Kama mpango huo sasa utawezekana, ni suala la kusubiri na kuona.

Jambo jingine ni kwamba mabishano hayo ya ndgu huko Gaza yanafanya mambo yawe rahisi kwa serekali ya waziri mkuu Olmert wa huko Israel. Badala ya kuibinya serekali hiyo ifuate njia ya kutaka amani, sasa Wapalastina wanaipa serekali hiyo ya Israel kila sababu kuendelea kukataa kuwa na mawasiliano, mazungumzo na kuwalainishia kamba. Hakika punde kutakuweko na tetesi kwamba Israel iko nyuma ya hali hii yote. Lakini, ikiwa ni hivyo, basi Israel itakuwa inachezea moto. Hapa mtu anayejimaliza mwenyewe ni Wapalastina wenyewe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com