Wanajeshi waasi wamesalim amri Philippines
29 Novemba 2007Matangazo
Manilla:
Wanajeshi kama 50 na polisi wameanzisha auasi mwengine dhidi ya rais Gloria Macapagal Arroyo .Polisi watiifu kwa rais huyo wameizingira Hotel Peninsula mjini Manilla ambako wanajeshi hao wamejifungia.Mashahidi wanasema jeshi linatumia gesi za kutoa machozi.Rais Arroyo amekua akikutana na baraza lake la usalama.Wanajeshi hao wanaoasi walitoroka mahakamani leo asubuhi ambako walikua wajibu mashtaka dhidi ya kushiriki kwao katika njama iliyoshinfdwa ya mapinduzi mwaka 2003.Habari za hivi punde zinasema wanajeshi hao wamesalim amri.