1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Myanmar wajiondoa kwenye mji muhimu wa mpakani

Bruce Amani
11 Aprili 2024

Askari wa utawala wa kijeshi wa Myanmar wamejiondoa kwenye ngome zao katika eneo moja muhimu ambalo ni kitovu cha kibiashara karibu na mpaka na Thailand kufuatia siku kadhaa za makabiliano.

https://p.dw.com/p/4efOc
Min Aung Hlaing
Mkuu wa Jeshi la Myanmar Min Aung HlaingPicha: Sefa Karacan/AA/picture alliance

Hatua hiyo ni pigo jingine kwa jeshi la Myanmar linalokabiliwa na shinikizo. Wapiganaji wa Karen National Union - KNU na makundi mengine yanayowapinga watawala wa kijeshi yalianzisha mashambulizi kwenye mji huo wa Myawaddy wiki hii.

Myawaddy ni muhimu kwa serikali ya kijeshi inayokabiliwa na uhaba wa fedha, ambapo bidhaa za thamani ya dola bilioni 1.1 zilipita kwenye mji huo kwa miezi 12 kufikia Aprili, kwa mujibu wa wizara ya biashara ya serikali ya kijeshi.

Myanmar yaushtumu Umoja wa Mataifa kwa madai ya upande mmoja ya ukiukwaji wa haki za binadamu

Myanmar imekuwa katika mgogoro tangu jeshi lilipoiangusha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia mwaka wa 2021, lakini jeshi limekabiliwa na hasara kubwa katika miezi ya karibuni.