1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Myanmar: UN imerekodi madai yasiokuwa na msingi dhidi yake

Tatu Karema
10 Aprili 2024

Watawala wa kijeshi nchini Myanmar, wameshtumu kile walichokiita madai ya upande mmoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu rekodi yake ya haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/4ebvI
Myanmar |
Wanajeshi wa Myanmar Picha: AFP/Getty Images

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Global New Light nchini humo, wizara ya mambo ya nje imesema azimio la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo wa Mataifa lililopitishwa wiki iliyopita kukosoa ukiukwaji wa kutisha wa haki za binadamu nchini humo lilijumuisha madai yasiokuwa na msingi na kwamba nchi hiyo inalipinga vikali.

Guterres "asikitishwa" na mauwaji Myanmar

Serikali hiyo ya kijeshi imeongeza kuwa haikupokea mawasiliano rasmi kuhusu uteuzi wa hivi karibuni wa mjumbe maalumu mpya wa Umoja huo kwa nchi hiyo Julie Bishop, aliyewahi kuhudumu kama waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Australia.

Hata hivyo, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema kwa kuwa uteuzi huo uliofanywa kupitia azimio la Baraza Kuu, haufuati taratibu za mashauriano kama maazimio ya Baraza la Usalama.