1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wanajeshi wa Marekani wapambana na wanamgambo wa Kishia karibu na Baghdad.

Ni wafuasi wa kiongozi wa dini wa kishia

Moqtada al-Sadr ambaye wanamgambo wake wamepambana na majeshi ya Marekani.

Moqtada al-Sadr ambaye wanamgambo wake wamepambana na majeshi ya Marekani.

Wanajeshi wa Kimarekani leo walipambana na wapiganaji wa Kishia katika mji mkuu wa Irak Baghdad ambapo watu 13 waliuwawa, ikiwa ni siku moja baada ya mapigano kati ya wanaharakati wa Al-Qaeda na kundi hasimu yaliosababisha vifo kadhaa. Wakati huo huo Abdel-Rahman Aref aliyekua rais wa Irak kabla ya kuangushwa katika mapinduzi yaliomuweka madareakani Saddam Hussein, amefariki dunia leo mjini Amman Jordan akiwa na umri wa miaka 91.

Mapigano makali leo kati ya wanajeshi wa Marekani na wanamgambo wa kishia yalitokea katika eneo la kaskazini-magharibi mwa mji mkuu Baghdad la Shuala na miongoni mwa watu 13 waliouwawa ni pamoja na wanawake wawili. Shuala ni moja kati ya ngome kuu za wanamgambo wakishia wa jeshi la Mahdi ambao ni watiifu kwa kiongozi wa kidini Moqtada al-Sadr mwenye kuipinga Marekani.

Duru za habari zinasema mapigano yalizuka mapema alfajiri, wakati helikopta za wanajeshi wa Marekani zilipowashambulia wanaharakati hao wakishia. Picha zilizopigwa na mwaandishi habari wa Shirika la habari la Ufaransa AFP zilionyesha gari moja likiwa limeharibiwa kwa mfululizo wa risasi na baadae maiti zilichukuliwa na amamia aya washia hadi kati kati mwa mji wa Najaf kwa mazishi huku wakipiga kelele kuiilani Marekani na kujipiga vifua katika kile kilichoonekana kuwa ni kuonyesha hasira zao kwa mauaji ambayo afisa mmoja wa wanamgambo hao alisema ni ya raia wasio na hatia. Waombolezaji walisafiri na maiti hadi najaf kwa taxi na mabasi wakibebea bendera za irak

Mapigano ya leo ayametokaea siku moja baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Al Qaeda kupambana na polisi na wanacahama wa kundi moja la Wasunni kaskazini magharibi mwa Baghdad mapigano hayo katika mji wa Kanan katika wilaya ya Diayala yaliasababisha watu 23 kuuwawa.Marekani inadai viongozi kadhaa wa kikabila katika jamii ya Wasunni wameanza kuyaunaga mkono majeshi ya muungano na ya Irak kupamaba na wanaharakati wa Al-Qaeda nchini Irak, wanaoshutumiwa na Marekani kuwa chanzo cha vurugu na machafuko ya mwagaji damu nchini humo.

Wakati huo huo rais wa zamani wa Irak Abdel-rahman Aref aliyepinduliwa zaidi ya miaka 35 na mapinduzi hayo kumuweka baadae Saddam Hussein madarakani , amefariki dunia mjini Amman Jordan akiwa na umri wa miaka 91. Aref alihamia Jordan baada ya uvamizi wa Irak 2003. Alishika madaraka 1963, miaka mitano baada ya kuangushwa utawala wa Kifalme na kaka yake Abdesalam Aref kushika Urais na kumteuwa Abdel-Rahman kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi. Alishika hatamu za uongozi baada ya kifo cha kaka yake katika ajali ya helikopta. Alikua rais wa tatu wa hadi 1968 alipoangusha katika mapinduzi yasiomwaga damu yaliofanywa na chama cha Baath na hatimae saddam Hussein kushika hatamu.

 • Tarehe 24.08.2007
 • Mwandishi Moahammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CH99
 • Tarehe 24.08.2007
 • Mwandishi Moahammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CH99

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com