Wanajeshi 2 wa Denmark wafariki kutokana na majeraha yao
30 Novemba 2007Matangazo
Wanajeshi 2 wa Denmark waliokuwa wakitumika nchini Afghanistan wamefariki kutokana na majeraha waliyopata wakati wa mapigano na wanamgambo wa Taliban.Mapambano hayo yalizuka, wanajeshi hao walipokuwa wakipiga doria katika Bonde la Juu la Geresk katika wilaya ya machafuko ya Helmand.Denmark imepoteza wanajeshi 9 nchini Afghanistan,tangu kupeleka vikosi vyake nchini humo mwaka 2002.