1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Msafara wa wanajeshi wa UN washambuliwa Kaskazini mwa Mali

Angela Mdungu
4 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema kuwa wanajeshi wake 15 wa kulinda amani waliokuwa wakiondoka Kaskazini mwa Mali wamejeruhiwa baada ya misafara yao kushambuliwa kwa mabomu ya kutegwa ardhini.

https://p.dw.com/p/4YOny
Sehemu ya wanajeshi wa kulinda amani wa UN wakiwa kwenye gwaride kabla ya kuondoka Mali
Sehemu ya wanajeshi wa kulinda amani wa UN wakiwa kwenye gwaride kabla ya kuondoka MaliPicha: Ishara S. Kodikara/AFP/Getty Images

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuwa walinda amani wanane waliojeruhuwa siku ya Jumatano, walisafirishwa kwa ndege na wako katika hali nzuri.

Ameongeza kuwa, wanajeshi wengine saba waliojeruhiwa Ijumaa baada ya gari lao kushambuliwa, wamesafirishwa pia kwa ndege ingawa hakuweka wazi kuhusu hali zao.

Soma zaidi:Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waondoka eneo la Kidal 

Kulingana na msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa, walinda amani hao wanaondoka Mali wiki kadhaa kabla ya tarehe iliyopangwa kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama.