1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wairak wakabidhiwa hatamu za usalama Basra

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcHJ

Basra:

Jeshi la Uengereza limewakabidhi hii leo wanajeshi wa Irak ulinzi wa jimbo la kusini la Basra.Kwa namna hiyo,majimbo yote manne yaliyokua hapo awali yakisimamiwa na wanajeshi wa Uengereza yanakutikana chini ya usimamizi wa wanajeshi wa Irak.Kwa mujibu wa duru za kijeshi,jimbo la Basra ni tulivu na hakuna tena wanamgambo katika eneo hilo ambalo ni miongoni mwa maeneo yenye utajiri mkubwa wa mafuta nchini Irak.Asili mia 80 ya mafuta yanayosafirishwa ng’ambo,yanapitia katika bandari ya Basra.Wadadisi wanahofia pasije pakatokea mapigano ya kuania madaraka kati ya makundi ya washiya wanaohasimiana..Wanajeshi 5500 wa Uengereza wamesalia bado kusini mwa IrakNa serikali ya Uengereza inapanga kupunguza wanajeshi elfu tatu hadi january mwakani.