1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wa Ujerumani wamuweka Rais Wullf kikaangoni

Hamidou Oummilkheir21 Desemba 2011

Kisa cha Rais wa Ujerumani-Christian Wulff cha kuchukua mkopo wa riba nafuu na pendekezo la Umoja wa Ulaya kutaka wenye kumaliza kidato cha sita wawe na nafasi ya kusomea ukunga na uuguzi ndizo mada kuu magazetini

https://p.dw.com/p/13Wya
German President Christian Wulff speaks during an inauguration and dismissal event for federal judges in Berlin, Germany, Monday, Dec. 19, 2011. Germany's governing parties rallied behind the country's president Sunday amid persistent criticism over a private loan he received before becoming head of state. Germany's opposition argues that President Christian Wulff needs to do more to explain a 500,000 euro (US $650,000) loan he received in 2008 from the wife of a wealthy businessman, apparently at below market rates, when he was governor of Lower Saxony state. (Foto:Michael Sohn/AP/dapd)
Christian Wulff ,rais wa shirikisho la jamhuri ya UjerumaniPicha: dapd

Tuanzie lakini na shinikizo linalozidi kumkaba rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Christian Wulff.Gazeti la "NORDWEST-ZEITUNG linaandika:
"Rais wa shirikisho amekawia kujitetea.Tamko lake la kwanza ambalo kimsingi lingebidi liwe la mwisho,halikutosha ,akabidi kutoa la pili.Kwasasa Christian Wulff anawaachia mawakili wake wajibu masuala chungu nzima ya waandishi habari-licha ya hayo lakini bado anaendelea kujihami.Majibu aliyotoa mwanzo yalionekana kana kwamba haamini kama ana hatia.Na wala haonyeshi kutambua ukweli kwamba viwango anavyotegemea wengine watavifuata,yeye binafsi havitekelezi.Kama Wulf anaitambua hali hiyo au la ndilo suala litakaloamua kuhusu mustakbal wake.



Gazeti la "Münchner Merkur linahisi mkakati unaofuatwa na rais wa shirikisho unajulikana.Ggazeti linaendelea kuandika:Badala ya kutilia maanani uzito wa tathmini ya kile kinachojulikana ka "kisa cha Wulff" na vipi kitamalizika-maelezo yanayitolewa na rais wa shirikisho yanafanana moja kwa moja na yale yanayotolewa na wengi wa wanasiasa wanaojikuta wamebanwa.Wanaliangalia neno "ukweli" kuwa ni geni,wanajigeuza paa,wakisikia kitu kidogo tu wanakimbia-wanayakubali yale tu ambayo tokea hapo hayawezi tena kukanushika."




Gazeti la Badische Neueste Nachrichten linahisi pengine kisa hiki ni dawa.Gazeti linaendelea kuandika: kila mzozo kuna fursa mpya nyuma yake.Kwa namna hiyo,mzozo huu umesaadif wakati muwafak kwa Christian Wulff.Rais wa shirikisho amesaliwa na miaka mitatu kurekebisha maoni ya watu dhidi yake.



Mada yetu ya pili magazetini inahusu pendekezo la Umoja wa Ulaya kuhusu wauguzi na wakunga.Gazeti la "Bild-Zeitung" linaandika:Mabwana wa mjini Brussels wamekuja na kipya....Anaetaka siku za mbele kuwa muuguzi au mkunga anabidi kwanza afanye Abitur-yaani mtihani wa kidato cha sita.Vipi?Abitur ndio kizingiti kwa kazi ambayo tokea hapo wajuzi wanakosekana?Hakuna anaepinga Abitur,lakini nhadi wakati huu mafunzo ya kazi yamekuwa yakitosdhja pia.Wagonjwa hawatohudumiwa vyema zaidi,watoto hawatozaliwa na afya nzuri zaidi eti kwasababu wauguzi na wakunga wana shahada za abitur kwenye madaftari yao.Hata bila ya abitur vijana wanastahiki kupata kazi nzuri nchini Ujerumani..Ukweli ni kwamba ulimwengu mzima unatumezea mate kutokana na mfumo wetu wa elimu ya ncha mbili-mafunzo ya kazi na ya shule.Mchanganyiko wa shule na mafunzo ya kazi unawapatia fursa wanafunzi wa shule ambazo hazina mitihani ya abitur,na wao pia kupata kazi ya maana.Na hali hiyo inastahiki kusalia hivyo hivyo siku za mbele pia.Bado kilichiosemwa na wahenga kina uzito:Penye nia opana njia."



.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Abdul-Rahman, Mohammed

Berlin/ Bundespraesident Christian Wulff spricht am Montag (14.11.11) im Konzerthaus in Berlin waehrend eines Festakts zum 50-jaehrigen Jubilaeum des Bundesministeriums fuer wirtschaftliche Zusammenarbeit und Entwicklung (BMZ). Erwartet wurden 1.200 nationale und internationale Gaeste. Das Ministerium entstand am 14. November 1961 mit der Ernennung des ersten Ministers fuer wirtschaftliche Zusammenarbeit. Foto: Clemens Bilan/dapd
Rais Christian WulffPicha: dapd