1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa hatarini kuteswa Marekani na Israel

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cuen

TORONTO: Hati iliytolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kanada siku ya Ijumaa imesema,wafungwa nchini Marekani na Israel wanakabiliwa na hatari ya kuteswa.Hati hiyo ni mwongozo wa mafunzo yanayotolewa kwa wanadiplomasia wa Kanada.

Afghanistan,China,Misri,Iran,Saudi Arabia,Mexico na Syria ni nchi zingine zilizotajwa katika waraka huo.Kanada imesema,hati hiyo ni kwa ajili ya kutoa mafunzo na wala haihusiki na sera rasmi ya serikali.