Waasi wauwa wanavijiji 12 Kivu ya kusini | Habari za Ulimwengu | DW | 27.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waasi wauwa wanavijiji 12 Kivu ya kusini

Wanavijiji 12 wamepigwa visu na kuuliwa jana usiku huko Kaniola-katika kivu ya kusini,kufuatia hujuma za waasi wa kihutu wa Rwanda katika eneo hilo la mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Gavana wa Kivu kusini,Célestin CIBALONZA ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP waasi wa FDLR-Forces Democratiques de Libération du Rwanda wamekishambulia kijiji cha Kaniola jana usiku na kuwauwa watu wasiopungua 12.Kijiji cha Kaniola kinakutikana Walungu umbali wa kilomita 50 magharibi ya Bukavu.Kwa miaka sasa kijiji hicho kimegeuzwa uwanja wa matumizi ya nguvu ,pakiwepo mashambulio,mali kuporwa na watu kutekwa nyara,yanayofanywa na waasi wa kihutu wa Rwanda na waasi wa “Rasta”kundi lililoundwa na wanamgambo wa kienyeji na kigeni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com