1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wakuu wa serikali mpya ya Kenya watembelea maeneo yaliyoathiriwa na ghasia kutokana na uchaguzi

25 Aprili 2008

Viongozi wakuu wa serikali mpya ya mseto nchini Kenya wanaendelea na ziara yao katika maeneo yaliyoathiriwa sana na ghasia zilizosababishwa na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

https://p.dw.com/p/Doft
Watu waliokimbia makaazi yao kutokana na ghasiaPicha: Picture-Alliance /dpa

Hapo jana viongozi hao Rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa rais Kalonzo Musyoka, walikuwa katika eneo la Eldoreti ambako inaarifiwa ya kwamba Rais Kibaki na Makamu wake walizomewa na wananchi.


Leo hii viongozi hao wako katika wilaya ya Kipkelion ambako kuna zaidi ya watu 1000 wanaoishi katika mahema baada ya kuyakimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo.


Aboubakary Liongo alizungumza na mwandishi wa habari wa Citizen anayefuatana na viongozi hao, Ngige Ngugi.