Viongozi wa kundi la FDLR wakamatwa nchini Ujerumani.
17 Novemba 2009Matangazo
Kalsruhe :
Polisi ya Ujerumani imewatia nguvuni viongozi wawili wa Kihutu ambao wameongoza harakati za waasi wanaoendesha visa vya ubakaji, mauaji na uharibifu mashariki mwa Congo.
Dr Ignace M mwenye umri wa miaka 46 ambaye ni rais wa kundi la waasi la FDLR anatakiwa nchini Rwanda kwa uhalifu wa kivita.
Maafisa wa Ujerumani wanalichukulia kundi hilo kuwa la kigaidi.
Mwingine aliyekamatwa ni Naibu wake anayejulikana kwa jina la Straton M mwenye umri wa miaka 48.
Mwendesha mashitaka wa Shirikisho alisema kuna ushahidi wa kutosha kuwa, wanahusika na uhalifu wa kivita.
Huenda wakafunguliwa mashtaka hapa Ujerumani.