Viongozi wa gazeti la Standard wahojiwa na polisi nchini Kenya
17 Aprili 2007Matangazo
Ndugu hao wawili maarufu kama "Kina Artur" wamekuwa wakitajwa na upinzani kuwa ni kitisho kwa usalama wa taifa baada ya kuonekana kuwa karibu na maafisa wa ngazi ya juu serikalini wakidaiwa kuwa na usemi katika baadhi ya mambo, waliamriwa kuihama Kenya mwishoni mwa mwaka jana.
Mmoja wa waliohojiwa jana ni mkurugenzi wa uhariri Kwendo Opanga ambaye alizungumza na Mohamed Abdulrahman.