1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Myanmar laombwa kuacha kuwashambulia raia wake

5 Septemba 2023

Viongozi wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia wamelaani hali ya kuongezeka machafuko na mashambulizi dhidi ya raia wa Myanmar wakielekeza lawama kwa utawala wa kijeshi uliochukua madaraka kwa nguvu mwaka 2021.

https://p.dw.com/p/4VzJY
Indonesia ASEAN
Picha: Mast Irham/AP Photo/picture alliance

Tamko la pamoja la viongozi hao, limetokewa katika siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya kikanda ya ASEAN unaofanyika kwenye mji mkuu wa Indonia, Jakarta ambao unatawaliwa na ajenda ya mzozo wa Myanmar

Katika tamko hilo lenye vipengele 19, viongozi hao wa kundi la mataifa kumi wamelitaka jeshi la Myanmar na wahusika wengine kukomesha mara moja makabiliano na kuwalenga raia au maeneo ya umma ikiwemo shule, masoko na hospitali. 

Ufilipino yajitolea kuiongoza ASEAN badala ya Myanmar

Ukosoaji huo unafuatia ripoti za makundi ya haki za binadamu zinazolituhumu jeshi kufanya mashambulizi holela kwa kutumia ndege za kivita kwenye ngome kuu za waasi wanaoupinga utawala wa majenerali.