1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VALENCIA : Repoti ya mabadiliko ya hewa kutolewa leo

17 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImG

Wataalamu wa hali ya hewa wanaokutana mjini Valencia nchini Uhispania wamekubaliana juu ya repoti kuhusu athari za ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na njia za kupambana na hali hiyo.

Jopo la Kiserikali juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa IPCC limeonya kwamba serikali duniani kote zina muda mchache tu uliobakia kujiepusha na taathira mbaya kabisa za mabadiliko ya hali ya hewa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatazamiwa kuzinduwa repoti hiyo baadae leo hii.

Jopo la IPCC linasema waraka wao huo utatumika kama muongozo na wanasiasa wanaokabiliwa na utowaji maamuzi juu upunguzaji wa uchafuzi wa hali ya hewa kutokana na nishati zinazoathiri mazingira,kutumia nishati safi na kuimarisha hatua za kupambana na mafuriko na majanga mengine ya asili ambayo yanatazamiwa kuwa makubwa zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kutolewa kwa repoti hiyo kunakuja kabla ya mkutano wa Bali nchini Indonesia ambapo mataifa duniani yatakutana hapo mwezi wa Desemba kutowa mpango wa kujadili upunguzaji wa utowaji wa gesi za carbon dioxide baada ya mwaka 2012 wakati mkataba wa Itifaki ya Kyoto utakapomalizika muda wake.