Utawala wa hali ya hatari kuondolewa Pakistan leo
15 Desemba 2007Matangazo
ISLAMABAD
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ametia saini agizo la kuondowa utawala wa hali ya hatari nchini humo.
Musharraf alitangaza utawala wa hali ya hatari mapema mwezi wa Juni kwa kusema kwamba alikuwa akichukuwa hatua hiyo kukabiliana na umwagaji damu unaoengezeka wa wanamgambo na vyombo vya mahkama vinavyoidhoofisha srikali.
Uchaguzi nchini Pakistan umepangwa kufanyika hapo tarehe nane mwezi wa Januari mwakani ambapo vyama vyote viwili vya mawaziri wakuu wa zamani Benazir Bhutto na Nawaz Sharrif vikitarajiwa kushiriki.