1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yashambulia kusini mwa mkoa wa Odesa

Zainab Aziz
17 Septemba 2023

Urusi imefanya mashambulizi nchini Ukraine kwa ndege zisizokuwa na rubani na makombora yaliyolenga zaidi maeneo ya kusini mwa mkoa wa Odesa na kupiga kiwanda cha bidhaa za kilimo.

https://p.dw.com/p/4WRLU
Zerstörte Getreidespeicher im Hafen von Odessa, Ukraine
Picha: Odesa Regional Administration Press Office/AP/picture alliance

Jeshi la anga la Ukraine limesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba Urusi imefanya mashambulizi sita ya droni za Shahed zinazotengenezwa Iran pamoja na makombora 10. Lakini jeshi la Ukraine lilifanikiwkukidungua droni sita na makombora sita kabla ya kuanguka kwenye maeneo yaliyolengwa. 

Jengo la Supermarket lililoshambuliwa katika mji wa Odesa
Jengo la Supermarket lililoshambuliwa katika mji wa OdesaPicha: OLEKSANDR GIMANOV/AFP/Getty Images

Hali kwenye mkoa wa Odesa na bandari zake imekua ikifuatiliwa kwa karibu na wanunuzi wa nafaka, baada ya Kyiv kusema jana Jumamosi kwamba meli za shehena zimewasili mkoani humo zikitumia ujia wa muda kufika kwenye bandari za Bahari Nyeusi ili kupeleka nafaka Afrika na Asia.

Wakati huo huo Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameiongezea shinikizo Ujerumani kwa kuitaka iongeze mchango wake wa ulinzi katika wakati huu wa vita vya Urusi nchini Ukraine.

Soma:Ujerumani yakaribia kufanya maamuzi ya kupeleka makombora ya kisasa kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi

Kwenye mahojiano na shirika la habari la Ujerumani Funke, Stoltenberg amekumbushia enzi ya Vita Baridi wakati makansela Konrad Adenauer na Willy Brandt walipochangia asilimia tatu hadi nne ya pato la taifa kwenye bajeti ya ulinzi.

Wakati huo huo Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesisitiza kwa kusema kama hilo liliwezekana wakati huo, ni lazima lifanyike tena sasa.

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens StoltenbergPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Muda mfupi baada ya Urusi kuivamia Ukraine, kansela Olaf Scholz aliahidi kiasi cha euro bilioni 100 ya bajeti ya mwaka 2022 kwa ajili ya matumizi ya kijeshi na pia aliahidi kufikisha asilimia mbili ya pato la ndani la Taifa kwenye matumizi ya ulinzi ya NATO.

Vyanzo:RTRE/DPA