1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ujerumani kuipa Ukraine makombora ya Taurus?

15 Septemba 2023

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema leo kuwa nchi hiyo ina wiki moja au mbili kabla ya kufanya maamuzi ya kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu aina ya Taurus.

https://p.dw.com/p/4WOEc
Kombora la masafa marefu la Taurus kama linavoonekana kwenye picha, ambalo huenda yakapelekwa Ukraine, ikwia Ujerumani itaridhia.
Kombora la masafa marefu la Taurus kama linavoonekana kwenye picha, ambalo huenda yakapelekwa Ukraine, ikwia Ujerumani itaridhia.Picha: Bernhard Huber/MBDA

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Münster, Pistorius ameeleza kuwa kuchelewa kwa uamuzi huo hakumaanishi kuwa, serikali ya Ujerumani haiko tayari kuipa Ukraine silaha bali inazingatia athari ambazo huenda zikajitokeza.

Ukraine kwa muda mrefu imeomba makombora kutoka Ujerumani yaliyo na uwezo wa kufanya mashambulio ya umbali wa hadi kilomita 500, ikisema inahitaji makombora hayo ili kukabili mashambulizi yanayofanywa na Urusi.

Ujerumani ina takriban makombora 500 aina ya Taurus, huku karibu nusu ya silaha hizo zikihitaji kufanyiwa ukarabati au kuboreshwa.

Hata hivyo Kansela Olaf Scholz ameonekana kusita kuipa Ukraine silaha zaidi kutokana na wasiwasi kwamba silaha hizo huenda zikazidisha vita.