Urusi na Marekani zabadilishana majasusi
9 Julai 2010Matangazo
Tangazo hilo limetolewa muda mfupi baada ya majasusi hao 10 kukiri kuwa na hatia mjini New York Marekani kwa makosa madogo ya kuwa mawakala wa serikali ya kigeni bila kibali.
Katika hatua inayohusiana na kesi hiyo, rais wa Urusi, Dmitry Medvedev amewasamehe majasusi wanne walioshtakiwa kwa kutoa habari za siri kwa nchi za magharibi.
Washukiwa hao walitakiwa na serikali ya Urusi kusaini taarifa kukubali makosa yao kama sharti la kuachiwa kwao. Makubaliano ya kubadilishana majasusi hao kati ya Marekani na Urusi yamefikiwa kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa.
Mwandishi:Josephat Charo
Mhariri:Aboubakary Liongo